Hapo zamani watu walikuwa wanamuona mtoa roho (Izraeli) anapokuja kuchukua roho zao.
Siku moja alienda kutoa roho ya jamaa mmoja aliyekuwa tapeli maarufu katika nchi ya misri. Mtoa roho alipofika akamwambia
Mtoa roho: kwa mujibu wa listi yangu hapa inaonekana kuwa leo ndio siku yako ya kufa
Tapeli: enheeeee! nashukuru kweli maana nilikuwa naisubiri hiyo siku kwa hamu na nilikuwa nashangaa kwa nini unachelewa kuja
Mtoa roho: basi mshukuru mungu wako nimefika
Tapeli: Kwa furaha niliyo nayo naomba nikununulie hata soda au maziwa unywe halafu tuendelee na kutoa roho yangu
Mtoa roho akakubali na kukaribishwa soda. Kumbe yule tapeli akamtilia
kilevi kikali katika soda. kisha mtoa roho alipolewa na kulala
akaichukua ile listi ya mtoa roho halafu akaliweka jina lake chini
kabisa tokea kule juu.
Baada ya muda yule mtoa roho akaamka baada ya kilevi kile kumuisha na kusema
Mtoa roho: Aisee kutokana na ukarimu uliouonyesha wa kunikaribisha kinywaji basi nitakupendelea ili usife leo
Tapeli: Kweli!?
Mtoa roho: ndio, nilipokuwa nimelala niliongea na
mungu na kumuomba ruhusa kuwa nisianzie juu kwenda chini katika orodha
yangu badala yake nianzie chini kwenda juu ili uwe wa mwisho na mungu
amenikubalia hivyo naomba listi yangu katika begi nijue nani wa chini
No comments:
Post a Comment
Comment here::