IBADA ZITAKAVYOKUWA MIAKA IJAYO

Miaka michache ijayo, ibada zitakuwa kama ifuatavyo.

MCHUNGAJI: Bwana asifiweee!
WAUMINI: Ameeen!
MCHUNGAJI: Tafadhalini washarika sasa tuchukue iPad,
tablet,Iphone na kindle zetu ili tufungue 1 Wakorintho
13:13. Pia washeni bluetooth zenu ili muweze kupokea mahubiri. Mnaotumia facebook, twitter, BBM na Whatsapp mnaweza kuendelea kupokea mahubiri haya. Tafadhalini
washarika mnaweza kutumia Wi-Fi ya kanisa kwa uhuru
kabisa kwa kutumia nywila/Password ya IMANI613. Haleluuyah!
WAUMINI: Haleluuuuyaaaaah!
MCHUNGAJI: Wapendwa washarika sasa ni wakati wa sadaka kwa hiyo kadri ya itakavyokupendeza kumtolea Mungu unaweza kutumia credit,Visa ama debit card, pia unaweza
kutoa sadaka kwa njia ya MPesa, Tigopesa, Airtel money ama EzyPesa kupitia namba zinazoonekana kwenye skrini.
 

WAKATI WA MATANGAZO :
KATIBU WA KANISA:(1) Wapendwa washarika wiki hii kutakuwa na mikutano ya kiroho kupigia group letu la Facebook. Mada kuu itakuwa uponyaji wa kiroho kwenye ndoa. Washarika wote mnakaribishwa kushiriki.(2) Siku ya Alhamisi kutakuwa na mafundisho ya Biblia moja kwa moja kupitia Skype kuanzia saa moja jioni. Tafadhali msikose kushiriki. Pia mnaweza kuendelea kufuatilia ibada hii pamoja na mafundisho yote kutoka kwa mchungaji kupitia akaunti yake ya Twitter.
Haleluyaaaaaah!
WAUMINI: Ameen!

No comments:

Post a Comment

Comment here::

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...