KACHEZE NJE!

Mtoto ( wa kiume) wa miaka minne alikuwa amekaa sebuleni na wazazi wake ambao walikuwa wametembelewa na rafiki zao ambao ni wanandoa (mke na mume). Wakati wa maongezi baba wa mtoto akawataarifu wageni wake kuwa rafiki yake (ambaye nao wanamfahamu) amebahatika kupata mtoto wa kike.
Basi yule mtoto baada ya kumsikia baba yake akisema rafiki yao amebahatika kupata mtoto wa kike, akamuuliza baba yake "Hivi baba mnajuaje kama huyu mtoto ni wa kike?" baba yake akamjibu kwa ukali "kacheze nje na wenzako"

No comments:

Post a Comment

Comment here::

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...