KALI JESHINI

Mwanajeshi mmoja alikuwa katika mafunzo ya  kufundishwa jinsi ya kulenga na kupiga bunduki.wakati wapo kambini yule jamaa aliitwa pamoja na wanajeshi wenzake kwa ajili ya majaribio.Walipofika akaanza kuitwa wa kwanza naye alifanikiwa kupiga pale alipoambiwa alenge.Naye wa2 alipiga ipasavyo,basi ikaendelea hivyo mpaka ilipofika zamu ya bwanamdogo ndipo ilipoanza kasheshe navyo ilikuwa kama ifuatavyo.Baada ya zamu yake kufika alipewa risasi 50 za mwanzo na hakuweza kupiga hata moja sehemu iliyotakiwa.Baada ya kutokea hayo mkuu wake alimkabidhi risasi nyingine 30,lakini cha kushangaza nazo pia alizikosa.kutokana na hasira nyingi mkuu wake alimpa risasi nyingine 20 na kumwambia kwamba aende msitu uliopo nyuma ya kambi na ajiue kwa risasi hizo.Jamaa alitii agizo na kuanza kuelekea msituni. Risasi zilisikika zikilia lakini baada ya muda mfupi yule jamaa alirudi akiwa mzima na mkuu wake alipomuuliza kwa nini hajafa alimjibu"Mkuu nimejikosa".Fikiria ungekuwa wewe ungefanyaje?

No comments:

Post a Comment

Comment here::

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...