Jamaa
alinunua friji jipya, akawaza namna ya kuondokana na lile la zamani
basi hatimae akaliweka nje ya nyumba yake na kuandika kibao ANAE TAKA
KUCHUKUA ACHUKUE BURE. Watu wakawa wanapita wanafungua lakini kila mtu
akawa anaogopa kuchukua maana hakuna aliyeamini mtu anaweza akagawa
friji zima bure. Baada ya kuona wiki imepita halijachukuliwa, akaandika
FRIJI INAUZWA LAKI 3, usiku
uleule likaibiwa.

No comments:
Post a Comment
Comment here::