BANGI NOMAA!
Usiku mmoja majira ya saa mbili usiku hivi washkaji wawili walikua wanatoka
kwenye kibarua chao cha kuchimba kisima wanaelekea makwao, walikua
wamevuta bangi kabla hawajatoka eneo la kazi, sasa wakiwa wanakatiza
vichochoroni watokee barabara kubwa wapate basi, siku hiyo ilikua na
mbalamwezi, mmoja akamuuliza mwenzake, hivi lile ni jua? akimaanisha ule
mwezi ulioandama, yule mwenzake akauangalia ule mwezi kwa makini kidogo
akitafakari alafu akamjibu rafiki yake, kwa kweli sina uhakika maana
mimi maeneo haya sio mwenyeji. wakaendelea na safari yao.
No comments:
Post a Comment
Comment here::