M-TZ NA MKENYA

Mtanzania na mkenya waliingia supermarket moja jijini DSM.Walipotoka nje,mkenya akawa anajigamba kwamba wakenya ni wajanja kuliko watanzania huku akimuonesha mtanzania chocolate tatu alizoiba supermarket.Mbongo akamshawishi mkenya warudi tena ndani ya supermarket ili naye akamuoneshe ustadi wake.Walipofika tu ndani,mtanzania akamwambia mhudumu,"nataka kukuonesha mazingaombwe,hebu niletee chocolate tatu!".Yule mhudumu akamletea chocolate tatu,jamaa akazila zote mbele ya mhudumu halafu akasema,"unaona mhudumu,mwenyewe umeshuhudia nimekula chocolate tatu lakini amini usiamini,chocolate zako ziko mfukoni kwa huyu jamaa".Mhudumu akamkagua mkenya mfukoni then akachukua chocolate zake zote tatu.Hahahaaa Teh! teh! teh!

No comments:

Post a Comment

Comment here::