M-TZ NA MKENYA
Mtanzania na mkenya waliingia supermarket moja jijini DSM.Walipotoka
nje,mkenya akawa anajigamba kwamba wakenya ni wajanja kuliko watanzania huku
akimuonesha mtanzania chocolate tatu alizoiba supermarket.Mbongo
akamshawishi mkenya warudi tena ndani ya supermarket ili naye
akamuoneshe ustadi wake.Walipofika tu ndani,mtanzania akamwambia
mhudumu,"nataka kukuonesha mazingaombwe,hebu niletee chocolate
tatu!".Yule mhudumu akamletea chocolate tatu,jamaa akazila zote mbele ya
mhudumu halafu akasema,"unaona mhudumu,mwenyewe umeshuhudia nimekula
chocolate tatu lakini amini usiamini,chocolate zako ziko mfukoni kwa
huyu jamaa".Mhudumu akamkagua mkenya mfukoni then akachukua chocolate
zake zote tatu.Hahahaaa Teh! teh! teh!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Comment here::